Dabi ya jijini la Mbeya, takwimu muhimu Mbeya City walizopanga kuzivunja

Ligi Kuu Soka Tanzania Bara inaendelea Jumapili Januari 14 kwa mchezo mkali wa Dabi ya jijini la Mbeya kati Wajelajela Tanzania Prisons na Mbeya City 'Wanakomakumwanya'.

Mchezo huo ambao utafanyika kwenye dimba la Kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya, unavuta hisia kwa wapenzi wa soka hapa nchini ukizingatia matokeo ya timu hizo mbili pindi zinapokutana.

Kwa miaka mitatu sasa Mbeya City wameshindwa kabisa kupata ushindi mbele ya Tanzania Prisons, jambo ambalo linazidi kutia chachu pambano hilo.

Mbali na kushindwa kupata ushindi Lakini pia Mbeya City hawajawahi kutikisa nyavu za Tanzania Prisons katika michezo minne iliyopita pindi timu hizo zilipokutana.

Kadhalika matokeo ya hivi karibuni ya Mbeya City pamoja na yale ya Tanzania Prisons yanazidisha uhondo wa mchezo huo kwani Mbeya City hawajapata ushindi katika michezo mitano mfulululizo iliyopita.

Kocha mkuu wa Mbeya City Ramadhan Nswazurimo amesema kwao wanaona ni wakati sasa behewa kugeuka na wanaona wakipata ushindi katika mchezo huo.

-Kwa kweli tumejiandaa vizuri, nimesikia tuna miaka mingi hatujawahi kupata ushindi dhidi ya Tanzania Prisons, nafikiri muda umefika sasa kubadili mwelekeo wa behewa, nahitaji ushindi katika mchezo huu, Nswazurimo amesema.

Kwa upande wake Katibu wa Tanzania Prisons Havintishi Abdalah amesema matokeo ya nyuma ya kuwafunga mara kwa mara ndio yanaleta ugumu wa mchezo huo na ndio maana wamejipanga kuhakikisha wanapata ushindi mapema. 

-Kuwafunga mara kwa mara isiwe kigezo cha kushinda kwa sababu hiyo ndio inayoleta ugumu kwani hawawezi kukubali kila siku kufungwa, lakini sisi kama Tanzania Prisons tumejipanga vizuri mno, mwalimu kawapanga vizuri wachezaji wake kwa hiyo tutashinda mechi bila tatizo lolote, Havintishi amesema.

Tanzania Prisons wapo katika nafasi ya sita wakiwa na alama 18 wakati Mbeya City wao wapo katika nafasi ya 12 wakiwa na alama 12.

Mechi zilizopita baina yao.

28 Januari 2017 Tanzania Prisons 2-0 Mbeya City FC.

17 Septemba 2016 Mbeya City FC 0-0 Tanzania Prisons.

07 Februari 16 Mbeya City FC 0-0 Tanzania Prisons.

19 Septemba 2015 Tanzania Prisons 1-0 Mbeya City FC.

Related news
related/article
Local News
VPL: Simba, Okwi wazidi kuchanja mbuga
12 Apr, 18:30
Local News
Kyombo afurahia kuitwa timu ya Taifa
12 Apr, 17:25
Local News
Juuko, Nyoni warejea kikosini kuwavaa Mbeya City
12 Apr, 13:20
Local News
CECAFA U17: Mirambo kutumia vijana wa U16
05 Apr, 21:10
Local News
CECAFA Women championships kufanyika mwezi ujao
04 Apr, 11:30