Azam ndio mabingwa wa Mapinduzi Cup

Timu ya Soka ya Azam ya Jijini Dar es Salaam imefanikiwa kutetea taji la mapinduzi Cup baada ya kuwafunga URA kwa penati 4-3 baada ya dakika 90 kumalizika kwa suluhu ya 0-0.

Mchezo huo ambao umefanyika katika uwanja wa Amaan Visiwani Zanzibar, ulikuwa mkali kwa dakika zote, huku mlinda mlango wa Azam Razak Abalora akichaguliwa kuwa man of the match.

Azam wakicheza soka la kitabuni waliweza kuisumbua vilivyo ngome ya URA kwa dakika zote 90 Lakini hawakuweza kufunga bao katika dakika 90.

Katika changamoto za penati mlinda mlango wa Azam FC Razak Abalora alipangua penati mbili na kuisaidia timu hiyo kutwaa ubingwa huo licha ya Bruce Kangwa kukosa penati kwa upande wa Azam iliyopanguliwa na Ali Yanzi wa URA.

Taji la nne. 

Hili linakuwa taji la nne kwa Azam kutwaa katika mashindano haya na kuweka rekodi ya kutwaa taji hilo mara nyingi zaidi toka lilipoanzishwa mwaka 1998.

Mabingwa waliopita. 

1998 Jamhuri Pemba.

2001 Polisi (Zanzibar).

2002 KMKM (Zanzibar).

2004 Young Africans (Dar-es-Salaam).

2005 Mafunzo.

2007 Malindi SC (Zanzibar).

2008 Miembeni SC (Zanzibar).

2010 Mtibwa Sugar (Turiani).

2011 Simba SC (Dar-es-Salaam).

2012 Azam (Dar-es-Salaam).

2013 Azam (Dar-es-Salaam).

2014 Kampala City Council (Uganda).

2015 Simba SC (Dar-es-Salaam).

2016 Uganda Revenue Authority.

2017 Azam (Dar-es Salaam).

2018 Azam FC 

Related news
related/article
Local News
VPL: Simba, Okwi wazidi kuchanja mbuga
12 Apr, 18:30
Local News
Kyombo afurahia kuitwa timu ya Taifa
12 Apr, 17:25
Local News
Juuko, Nyoni warejea kikosini kuwavaa Mbeya City
12 Apr, 13:20
Local News
CECAFA U17: Mirambo kutumia vijana wa U16
05 Apr, 21:10
Local News
CECAFA Women championships kufanyika mwezi ujao
04 Apr, 11:30