Azam Vs URA, Himid Mao awaomba watanzania kuungana

Nahodha wa timu ya soka ya Azam Himid Mao Mkami amewaomba watanzania wote bila kujali timu wanazoshabikia kuwaunga mkono wakati wakienda kupambana na URA katika mchezo wa fainali wa mashindano ya Mapinduzi.

Akizungumza na mtandao masaa machache kabla ya mtanange huo kuanza, Himid ambaye amejumuishwa kwenye kikosi kitakachoanza amesema ni wakati sasa watanzania wakaungana na ili kuweza kuibuka na ushindi katika mchezo huo.

-Kwanza namshukuru Mungu tumeamka salama na tumefanya maandalizi mazuri, ni imani yetu tutapambana na kombe litabaki hapa hapa Tanzania, kwa mashabiki wa mpira nawaomba waje kwa wingi na waisupport timu ili tuweze kuondoka na ushindi, amesema.

Aidha katika kikosi kilichotangazwa na kocha Mromania Aristica Cioaba, kimekuwa na mabadiliko kidogo ukiondoa kile ambacho kilicheza na URA katika mchezo wa makundi na kuchapwa bao 1-0.

Cioaba amemuanzisha mlinda mlango Razak Abalora badala ya Benedict Haule ambaye hayupo kabisa hata katika wachezaji wa akiba, huku Benard Arthur akipewa nafasi nyingine ya kuanza mbele ya kinda Shaban Idd Chilunda.

Kikosi kinachoanza: Razak Abalora 16, Himid Mao 23, Bruce Kangwa 26, Agrey Moris 6, Yakubu Mohammed 5, Abdallah Kheri 25, Stephan Kingue 27, Frank Domayo 18, Salmin Hoza 22, Benard Arthur 9 na Yahya Zayd 52

Akiba: Mwadini Ali 1, David Mwantika 12, Braison Raphael 4, Iddi Kipagwile 21, Joseph Mahundi 17, Enock Atta 10, Salum Abubakar 8, Paul Peter 51 na Shabani Iddi 43.

Takwimu muhimu.

Mchezo huo wa fainali utafanyika kuanzia majira ya saa 2:15 usiku ambapo kama Azam wataibuka na ushindi basi watakuwa wamejiwekea historia ya kwao wenyewe ya kutetea taji hilo kwani waliwahi kufanya hivyo mwaka 2012 na 2013.

Mwaka 2012 Azam waliingia fainali na kuifunga Jamhuri Pemba kwa mabao 3-1 wakati mwaka 2013 walichukua taji kwa kuichapa Tusker FC ya Kenya mabao 2-1.

Kwa Upande wa URA kama watafanikiwa kutwaa taji, litakuwa ni taji la pili baada ya lile walilolitwaa mwaka 2016 kwa kuwafunga wakata miwa wa Turiani mkoani Morogoro Mtibwa Sugar kwa mabao 3-1.

Related news
related/article
Local News
VPL: Simba, Okwi wazidi kuchanja mbuga
12 Apr, 18:30
Local News
Kyombo afurahia kuitwa timu ya Taifa
12 Apr, 17:25
Local News
Juuko, Nyoni warejea kikosini kuwavaa Mbeya City
12 Apr, 13:20
Local News
CECAFA U17: Mirambo kutumia vijana wa U16
05 Apr, 21:10
Local News
CECAFA Women championships kufanyika mwezi ujao
04 Apr, 11:30