Mapinduzi Cup: Simba waitahadhalisha URA

Meneja msomi wa kikosi cha wekundu wa Msimbazi Simba SC Richard Robert amesema wanatambua umuhimu wa mchezo dhidi ya watoza ushuru wa Uganda URA kwenye michuano ya Mapinduzi Cup.

Robert amesema mchezo huo ni kama karata yao ya mwisho na kwa maana hiyo wamejipanga kuhakikisha wanapata ushindi na kutinga nusu fainali ya michuano hiyo.

-Tunaomba mashabiki wetu watuombee dua kwa kweli tunategemea kupata matokeo mazuri, kwa kuwa tunajua kabisa huu ndo mchezo wa mwisho, kwa hiyo tutapambana kufa na kupona, Robert amesema.

Razak Abalora 

Akizungumzia kuhusu matokeo ya mchezo dhidi ya Azam FC ambao walipoteza kwa bao 1-0, Robert amesema hata wao hawafahamu ni sehemu gani walitereza kwani walicheza vizuri kwa kutengeneza nafasi nyingi tofauti na Azam.

Robert amekiri kuwa sifa zote katika mchezo huo zimwendee mlinda mlango wa Azam Razak Abalora ambaye aliwanyima ushindi Kwa kiasi kikubwa zaidi katika mchezo huo.

-Mtu yoyote ambaye aliangalia ule mchezo, timu ilicheza ilifanya kila kitu, tulishambulia vibaya sana lakini hata kocha mwenyewe amesema yule kipa wa Azam ndiye aliyewasaidia Azam kuweza kushinda mchezo ule, amesema.

Ushindi wowote. 

Simba SC watajitupa uwanjani kucheza na URA katika mchezo wa kukamilisha hatua ya makundi, mchezo ambao utafanyika kwenye uwanja wa Amaan kuanzia saa kumi jioni.

Simba watahitaji ushindi wa aina yoyote ile ili kupata nafasi ya kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo itakayofikia tamati Januari 13 mwaka huu.

Related news
related/article
Local News
VPL: Simba, Okwi wazidi kuchanja mbuga
12 Apr, 18:30
Local News
Kyombo afurahia kuitwa timu ya Taifa
12 Apr, 17:25
Local News
Juuko, Nyoni warejea kikosini kuwavaa Mbeya City
12 Apr, 13:20
Local News
VPL: Yanga vs Singida United, vikosi vyawekwa wazi
11 Apr, 13:05
Local News
Lwandamina adaiwa kuikacha Yanga na kurejea Zesco United
10 Apr, 17:35