Samatta aanza mazoezi na wenzake

Mshambualiaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Ally Samatta amethibitisha kuanza mazoezi ya uwanja na timu yake ya KRC Genk ya Ubeligiji baada ya miezi miwili toka alipopata majeraha ya Goti.

Samatta ameandika katika ukurasa wake wa Instagram kuwa anamshukuru Mungu kwa kurejea tena uwanjani baada ya kukaa muda mrefu akiuguza jeraha la goti.

-Nina furaha, kuanza mazoezi ya uwanjani baada ya kuwa nje kwa takribani miezi miwili kutokana na maumivu ya goti, ameandika.

Toka Novemba 4

Samatta alipata maumivu kwenye mishipa midogo ya goti lake la mguu wa kulia ambayo ilichanika Novemba 4, mwaka jana akiichezea KRC Genk katika mchezo ambao ililazimishwa sare ya 0-0 na Lokeren kwenye mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza katika Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk.

Samatta aliumia akiichezea mechi ya 70 Genk tangu alipojiunga nayo Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Na katika mechi hizo 70, Samatta, mshambuliaji wa zamani wa Mbagala Market, African Lyon na Simba za Tanzania, amefunga mabao 22 kwenye mashindano yote.

Related news
related/article
Local News
Njombe Mji: Yajayo dhidi ya Simba yawafurahisha
02 Apr, 16:49
Local News
AWCON 2018: She-Polopolo watua na mziki mnene kuwakabili Twiga Stars
02 Apr, 08:23
Local News
Azam Fc wakubali matokeo wahamishia nguvu kwenye ligi kuu
01 Apr, 19:45
Local News
ASFC: Singida United waangusha mbuyu, watinga nusu fainali
01 Apr, 18:10
Local News
ASFC: Stand United wajitapa kunyakuwa ubingwa
01 Apr, 12:03