Elius Maguri ajiunga na Polokwame City ya Afrika Kusini

Mshambuliaji Mtanzania Elias Maguri amezipiga chini ofa za Simba na Yanga na klabu nyingine zilizokuwa zinamwania katika dirisha dogo la usajili, na kukamilisha uhamisho wake wa kujiunga na Polokwane City inayoshiriki Ligi kuu ya Afrika Kusini (PSL).

Maguri amejiunga na Polokwane City akiwa mchezaji huru baada ya kuvunja mkataba wake na klabu yake ya Dhofar FC ya Oman aliyojiunga nayo Juni Mwaka Jana akitokea Stand United 'Chama la wana' yenye makazi yake mkoani Shinyanga.

Abdi Banda. 

Maguri sasa anaungana na Abdi Banda anayeichezea Baroka FC ya Afrika Kusini, pamoja na mlinda mlango Deogratius Munish 'Dida'.

Dili la Maguri limekamilika akiwa na timu ya taifa ya Tanzania bara 'Kilimanjaro Stars' inayoshiriki michuano ya kombe la CECAFA CUP nchini Kenya.

Maguri amewahi kuvichezea vilabu vya hapa Tanzania kama Tanzania Prisons, Ruvu Shooting, Simba na Stand United.

Related news
related/article
Local News
VPL: Simba, Okwi wazidi kuchanja mbuga
12 Apr, 18:30
Local News
Kyombo afurahia kuitwa timu ya Taifa
12 Apr, 17:25
Local News
Juuko, Nyoni warejea kikosini kuwavaa Mbeya City
12 Apr, 13:20
Local News
CECAFA U17: Mirambo kutumia vijana wa U16
05 Apr, 21:10
Local News
CECAFA Women championships kufanyika mwezi ujao
04 Apr, 11:30