Mtanzania alichoka soka la Marekani, ataka kujiunga na Samatta.

Mwanasoka Yusuph Juma anayecheza soka nchini Marekani katika klabu ya Monroe SC, yuko kwenye maandalizi ya kwenda kufanya majaribio katika klabu za Standard Liège na R.S.C. Anderlecht za nchini Ubelgiji.

Yusuph ambaye ni mzaliwa wa Kigoma, kama atafanikiwa kujiunga na moja ya timu hizo, atakuwa Mtanzania wa pili kucheza Ligi Kuu Ubelgiji ‘Jupiler pro’ baada ya nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta anaichezea KRC Genk.

Akizungumzia na Gazeti la Mwanaspoti Yusuph amesema kama Ndiye aliyetengeza dili hilo na anatarajiwa kwenda Barani Ulaya kufanya mazungumzo na majaribio kwa ajili ya kujiunga na timu za England na Ubeligiji.

-Kaka yangu ambaye ananisimamia kama wakala, amefanya mazungumzo na kufanikiwa kupata zaidi ya nafasi nne za majaribio, nitaanzia England na kumalizia, Ubelgiji,"anasema Yusuph.

Soka la Marekani. 

Amesema kwa sasa anacheza soka nchini Marekani na hilo linazidi kumpa imani kubwa ya kufuzu kwenye majaribio hayo na hatimaye kucheza soka Barani Ulaya.

-Nacheza ngazi ya juu kabisa ya soka la Marekani upande wa vyuo, baada ya hapo nitaingia kwenye mchakato wa kucheza ligi kuu, binafsi sivutiwi na ligi kuu ya hapa Marekani, ndiyo maana naenda kufanya majaribio huko Ulaya, Yusuph ameongeza.

Yusufu ambaye anazaidi ya miaka mitano nchini Marekani anasimamiwa na kaka yake, Hamisi pamoja na mdogo wake ambaye yupo kwenye kituo cha kulelea vipaji nchini humo cha New England Revolution.

Related news
related/article
Local News
Njombe Mji: Yajayo dhidi ya Simba yawafurahisha
02 Apr, 16:49
Local News
AWCON 2018: She-Polopolo watua na mziki mnene kuwakabili Twiga Stars
02 Apr, 08:23
Local News
Azam Fc wakubali matokeo wahamishia nguvu kwenye ligi kuu
01 Apr, 19:45
Local News
ASFC: Singida United waangusha mbuyu, watinga nusu fainali
01 Apr, 18:10
Local News
ASFC: Stand United wajitapa kunyakuwa ubingwa
01 Apr, 12:03