Raja Casablanca wakatisha ndoto ya Simon Msuva.

Winga machachari nchini, Saimon Msuva amepoteza nafasi ya kushinda taji la kwanza nchini Morocco baada ya timu yake ya Difaa El Jadida kufungwa na Raja Casablanca kwenye fainali ya Kombe la Mfalme Jumapili.

Difaa ilitinga hatua ya fainali baada ya kuifunga RSB Berkane kwa matokeo ya jumla, mabao 4-3.

Raja Casablanca ambao wamechukua ubingwa huo kwa kuifunga timu ya Msuva penati 3-1 ambapo Casablanca wao walitinga hatua hiyo kwa kuwaondoa FAR Rabat kwa faida ya bao la ugenini.

-Kuna muda mipango inaweza isiwe matumizi, tulicheza vizuri mwanzo hadi mwisho wa mchezo, Walianza kutufunga kipindi cha kwanza, lakini tulisawazisha kipindi cha pili, kwenye penati tukapoteza, siku zote penati hazina mwenyewe, Msuva aliliambia Gazeti la Mwanaspoti.

Nguvu kwenye ligi. 

-Kilichobaki ni kuelekeza nguvu kwenye ligi, kule napo inawezekana tukafanya vizuri japo ingependeza zaidi kama tungeshinda Kombe la Mfalme ila ndiyo hivyo imeshatokea, alisema Msuva.

Katika mchezo huo Msuva aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Adnane El Ouardy.

Related news
related/article
Local News
VPL: Simba, Okwi wazidi kuchanja mbuga
12 Apr, 18:30
Local News
Kyombo afurahia kuitwa timu ya Taifa
12 Apr, 17:25
Local News
Juuko, Nyoni warejea kikosini kuwavaa Mbeya City
12 Apr, 13:20
Local News
CECAFA U17: Mirambo kutumia vijana wa U16
05 Apr, 21:10
Local News
CECAFA Women championships kufanyika mwezi ujao
04 Apr, 11:30