Streka Thomas Ulimwengu apata tumaini jipya.

Mshambualiaji wa kimataifa wa Tanzania Thomas Ulimwengu, anaweza kurejea uwanjani hivi karibuni baada ya kuonekana kwenye mtandao wake wa Instagram akijifua vilivyo katika nchi moja barani Ulaya.

Kwa sasa Ulimwengu amekuwa akifanya mazoezi binafsi ya uwanjani baada ya kuruhusiwa na daktari wake aliyemhakikishia ataanza kucheza mechi za ushindani Januari mwakani.

Ulimwengu ambaye anakipiga katika timu ya AFC Eskilstuna ya Sweden lakini ameshindwa kabisa kujiunga nao toka alipofanyiwa upasuaji mwezi Julai mwaka huu.

-Namshukuru Mungu naendelea vizuri, nimeanza kufanya mazoezi ya uwanjani ya kwangu binafsi, kwani awali nilikuwa nafanya ya viungo tu,” alisema Ulimwengu kwa njia ya simu alipozungumza na Gazeti la Mwanaspoti.

-Hata hivyo sijajiunga na klabu yangu na sipo Sweden, kuna nchi nimejificha huku huku Ulaya najiweka sawa kwanza na daktari wangu ameniambia, nitarudi uwanjani kuanza kucheza Januari mwakani," Amesema.

Hajacheza muda mrefu. 

Ulimwengu ambaye ni straika tegemeo wa Taifa Stars, alikaa nje ya uwanja baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti nchini Afrika Kusini na anaamini atakuwa sawa mapema na kurudi uwanjani.

Maumivu ya goti yamekuwa yakimsakama Ulimwengu tangu alipojiunga na Eskilstuna Januari mwaka huu akitokea Tout Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kiasi cha kushindwa kucheza.

Related news
related/article
Local News
VPL: Simba, Okwi wazidi kuchanja mbuga
12 Apr, 18:30
Local News
Kyombo afurahia kuitwa timu ya Taifa
12 Apr, 17:25
Local News
Juuko, Nyoni warejea kikosini kuwavaa Mbeya City
12 Apr, 13:20
Local News
CECAFA U17: Mirambo kutumia vijana wa U16
05 Apr, 21:10
Local News
CECAFA Women championships kufanyika mwezi ujao
04 Apr, 11:30